Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza,, kikao cha kitaifa kuhusu Palestina kimefanyika kwa juhudi za Baraza la umoja wa umma wa kiislamu la Pakistan, kikiwa na ushiriki mpana wa maulamaa mashuhuri na viongozi wa kidini katika kituo cha kitamaduni cha urafiki kati ya Pakistan na China huko Islamabad. Kikao hiki kilifanyika kwa lengo la kuchunguza hali ya Ghaza, kutangaza mshikamano na taifa la Palestina, na kubainisha majukumu ya umma wa kiislamu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni.
Maulamaa waliokuwepo kwenye kikao hiki, sambamba na kulaani jinai za wazi zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, walitangaza kuwa jihadi dhidi ya Israel imefaradhishwa kwa serikali na umma wa kiislamu. Pia walitaka kuzuiwa kwa ukamilifu bidhaa na makampuni yanayounga mkono utawala wa Israel, na wakasisitiza kuwa lazima kusimama kwa wingi dhidi ya uvamizi wa wazayuni.
Maoni yako